Katika hali ya kushangaza, mtoto Focus Saimoni (9), mkazi wa Kwa Bibi Yuda, Kinondoni jijini Dar amekutwa amejinyonga kwenye komeo la mlango wa sebule yao.
Focus aliyekuwa akisoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi
Kumbukumbu, amedaiwa kufanya tukio hilo Jumamosi iliyopita kwa kufunga
gauni la mdogo wake shingoni na kujitundika kwenye komeo hilo mpaka
kukata roho.
Kwa mujibu wa chanzo makini, tukio hilo
lilitokea saa 6 mchana wakati wazazi wa mtoto huyo wakiwa kazini na
kuacha ufunguo kwa mmiliki wa nyumba aliyejulikana kwa jina la mama
Fau.Chanzo hicho kilieleza kuwa siku ya tukio, Focus alirejea nyumbani
kutoka shuleni na kumuacha mdogo wake, Irene Steve (5).
“Alipofika alichukua ufunguo kwa mama mwenye nyumba na kuingia
ndani, akanywa chai. Baada ya muda, mdogo wake (Irene) alirudi na
kumkuta tayari ananing’inia kwenye komeo la mlango,” kilisema chanzo.
Akizungumzia tukio hilo, mtoto Irene alisema baada ya kumkuta Fucus akining’ing’inia hakuamini mara moja kama amefariki dunia.
“Nilimwambia Focus usinitanie mbona hauzungumzi na mimi,
nilipomwangalia vizuri ndipo nikaona ana damu mdomoni, nikakimbia kwa
mama mdogo anayeishi jirani na kumueleza,’’ alisema Irene.
Akizungumza na mwandishi wetu, mama mdogo wa Irene, Catherine Zakaria
alisema naye hakuamini tukio hilo.
“Aliponiambia Focus kaning’inia mlangoni nilishtuka, nikakakimbilia eneo la tukio na kukuta kweli.
“Ila mimi naamini kuna mtu alimnyonga kwa kutumia gauni la ndugu yake, nasema wamemnyonga kwa sababu mazingira ya tukio asingeweza kujitundika juu ya komeo mwenyewe kwa umri wake na kimo chake,’’ alisema Catherine.

Akizidi kufafanua juu ya mazingira
aliyoyakuta, Catherine alisema alishangaa wakati akihangaika kuita
majirani, aliporudi aliukuta mwili umeshushwa chini.
“Niliukuta mwili wa marehemu ukiwa umening’inia juu ya mlango lakini katika kutoka kuita majirani, kurudi nikakuta mwili umeshushwa chini, nilipojaribu kuuliza ni nani aliyeushusha, hakuna aliyenijibu,’’ alisema Catherine.
Akizungumzia tukio hilo, mmiliki wa nyumba hiyo, mama Fau, alisema alishtushwa na tukio hilo.

’’Tukio hili lina shaka ndani yake, mtoto wa miaka 9 anawezaje
kujinyonga, kwa stress zipi? Kwa kweli inasikitisha sana, jeshi la
polisi lina wajibu wa kuchunguza ukweli wa kifo cha mtoto huyo,” alisema
mama huyo.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo pia walionekana kushtushwa na tukio hilo na kuwauliza wazazi kama mtoto huyo alikuwa na stress zozote?
Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo pia walionekana kushtushwa na tukio hilo na kuwauliza wazazi kama mtoto huyo alikuwa na stress zozote?
Mama wa marehemu, Rehema alisema anaumia kukuta mwanaye amefariki dunia na kuomba vyombo vya dola vifanye kazi yake kikamilifu.