Mwanasheria mkuu wa chama
Demokrasia na maendeleo Chadema Bw Tundu Lisu amesema baada ya Mh
Rais Dr.Jakaya Kikwete kukubali kupokea katiba iliyopendekezwa na
bunge la katiba, kazi kubwa waliyonayo kama chama cha upinzani
ni kuwaelimisha wananchi kuyaona madhaifu yaliopo kwenye rasimu
ya katiba hiyo ili waweze kuikataa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika jijini
arusha Bw. Lisu amesema hatua iliyofikiwa sasa hatma ya katiba hiyo
iko mikononi mwa wananchi na watafanya kila wanaloweza
kuwaelimsha na kuwashawishi wananchi kuikataa.
Aidha Bw Lisu ambaye ni mnadhimu mkuu wa chama hicho amesema
uchache wa wabunge wa upinzani ndio uliwezesha mchakato wa
katiba kufikia hatua iliyopo sasa huku ikibeba maslahi ya
wachache ,na kwamba kwa vile watanzania ni wengi kuliko
wachache wanaoshikilia mchakato huo chadema ina imani kubwa kuwa
haitapata kibali cha wananchi ili mchakato huo uweze kuanza
upya na kupatikana kwa katiba yenye maslahi ya wengi.
Awali mwenyekiti wa Chaedema mkoa wa Arusha Bw. Amani Golugwa
amewataka wananchi hasa vijana kuhakikisha wanajiandikisha na pia
wanajitokeza kwenye uchaguzi zote zilizoko mbele yao ukiwemo wa
serikali za mitaa kwani ndio njia pekee ya kuwawezesha kufikia
maamuzi wanayoyataka.
Kwa mujibu wa viongozi hao chama hicho kiko kwenye kampeni za
kufanya mikutano kila kata kuhamasisha wananchi kuyaelewa mapungufu
yaliyopo kwenye katiba iliyopendekezwa kuwashawishi kuikataa.