Kesi ya utekaji iliyokuwa ikimkabili Madee imemalizika kwa kulipa faini ya shilingi 50,000. Madee alidaiwa kumteka kijana mmoja huko Kigamboni baada ya kumuibia simu. Hakimu ametoa hukumu ya kifungo cha jela miezi sita au kulipa faini ya kiasi hicho cha fedha. Madee alilipa faini.
Madee amezungumza kwa mara ya kwanza tangu apatwe na mkasa huo.
“Yule dogo baada ya kuniibia simu tulimgonga kwa nyuma akaanguka
tukamwokota na kumbeba kwenye Noah yetu tukaondoka naye. Kesho yake
nilikuwa na safari ya kwenda Mwanza kwahiyo nikaachia masela wampeleke
polisi na hapo mimi nilishampigia simu mama yake ili aongee na mwanae
aseme simu yangu iko wapi. Simu yangu yenyewe ndio ilikuwa kila kitu.
Kwahiyo nilivyoondoka nikiwa sina hata mawasiliano, nikaenda Mwanza
nimefanya show, nimerudi Jumatatu asubuhi nikaulizia mtuhumiwa wangu
nikaambiwa yupo Magomeni. Nikaenda Magomeni polisi nikaambiwa dogo
kahamishiwa Kigamboni,” amesimulia Madee.
“Nikaamua kwenda Kigamboni, kwenda Kigamboni nikaambiwa ‘bwana wewe
ndo unashtakiwa ukitaka kumteka huyu dogo’ ndio nikawekwa ndani,
nikalala siku moja, asubuhi nikadhaminiwa nikatoka kesi ikaenda
mahakamani. Mahakamani kesi ikaahirishwa siku ya kwanza siku ya pili
ikapita, hukumu nikaambiwa kati ya kwenda jela miezi sita au kulipa
faini 50,000. Nikalipa faini na kesi ikaisha. Yaani mimi ndo nimekuwa
mwenye kosa, mimi ndo niliyelipa faini.”