WANAODHANIWA KUWA MAJAMBAZI WAUA ASKARI WAWILI BAADA YA KUVAMIA KITUO CHA POLISI, WATATU WAJERUHIWA

 
KAMANDA WA POLISI MKOANI GEITA JOSEPH  KONYO
BREAKING NEWS;
KITUO  cha polisi kilichopo Ushirombo wilayani Bukombe  mkoani Geita  kimevamiwa  na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi usiku wa saa tisa kuamkia leo  huku  askari wawili wakiuwawa na watatu wakijeruhiwa  vibaya 
 
Ambapo taarifa za awali  kupitia kwa mwandishi wa blog hii  ametaarifiwa kuwa licha ya matukio hayo  wamelipua  chumba cha kuwekea silaha  na zingine kuondoka nazo,pia wamefanikiwa kuondoka na  bunduki zaidi ya 5  aina ya SMG na kutokomea nazo .
 
Watu wamekusanyika  kituoni hapo  kushuhudia huku kituo hicho  kikiwa kimezungushiwa   kamba nyekundu kwa kusitisha huduma  na mahabusu  waliokuwemo wamehamishwa.
 
Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi  mkoani Geita Joseph Konyo yupo katika eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi .
 
Taarifa kamili itaendelea kutolewa kupitia blog hii.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo