Akizungumza katika Exclusive Friday ya 100.5 Times Fm, Gardner
ameeleza kuwa hizo ni taarifa zisizo za kweli ambazo amekuwa akizisikia
tu.
“Hakuna tatizo. Kusema ukweli nimekaa na Lady Jay Dee kwa miaka mingi
sana na hii sio mara ya kwanza kuzungumzwa kwa mambo kama hayo. Na
tumeshazoea.
Hata kama kuna kitu kinazungumzwa, mimi hata sina habari
kwa sababu nimeshazoea. Kwa hiyo na mimi pia nimesikia kama ulivyosikia
wewe. Lakini tatizo hakuna.” Amesema Gadner.
Ameeleza kuwa chanzo cha tetesi hizo kinaweza kuwa siku ambayo yeye
alionekana polisi katika kesi ya usalama barabarani na Lady Jay Dee
hakufika.
Amesema huenda watu walichukulia tofauti lakini ukweli ni kwamba yeye ndiye aliyemshauri asiende ili kuepusha attention zaidi.
“Na kwa watu kuzungumza…unajua Jay Dee ni mtu mashuhuri, ni
mkubwa sana. Kiasi kwamba kitu kidogo tu kikitokea, hata akijikwaa
kinazungumzwa kwa ukubwa huo.
Kwa mfano mimi nimepata shida kidogo ya
kesi ya traffic, kwa hiyo nikamshauri mwenzangu asije pale polisi kwa
sababu ya kuogopa tu vitu kama mapicha na nini. Kumbe watu walinotice
kwamba hakuja.
Kuanzia hapo ndio ikaanza ‘aah kuna tatizo..kuna tatizo’.
“Lakini kwa kweli kuzungumzwa kwa msanii mkubwa kama yule ni
jambo la kawaida. Na ni jambo ambalo ameshalizoea na mimi nimeshalizoea
pia.”
Hivo karibuni Jide alipost picha ya mkono inayoonesha pete yake ya
ndoa kumaanisha uimara wa ndoa yao tofauti na kilichokuwa kikisemwa.