VETA WASAJILI VYUO 19 TU KWA MKOA WA NJOMBE

Mamlaka ya mafunzo ya ufundi stadi VETA kanda ya nyanda za juu imetoa vyeti  kwa vyuo 19 vya mkoa wa Njombe   baada ya kupata usajili wa awali ambao utadumu kwa miaka miwili  na kuwataka wamiliki wa  vyuo hivyo kufundisha fani walizosajiliwa sambamba na kuhakikisha  wanaongeza fani za masomo katika vyuo vyao.

Akiongea katika makabidhiano ya vyeti hivyo kaimu mkurugenzi wa VETA nyanda za juu kusini Bi Susan  Magani amesema kuwa  kila mmiliki wa chuo anatakiwa kutoridhika na idadi ya fani anazotoa kwani ananafasi ya kusajili nyingine ili kuendana na mahitaji katika jamii kwa wakati husika

Naye mratibu wa mafunzo kanda nyada za juu John Mwanja   amewataka wamiliki wa vyuo hivyo kutambua tofauti ya madaraja, na kuacha tabia ya kufaulisha wanafunzi kwenye vyuo vilivyosajiliwa  sambamba na kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa kutoa taarifa ya kutokuwepo kwa vyuo visivyosajiliwa huku akieleza kuwa usajili huo ni hatua ya kuanza kupambana na vyuo feki katika kanda.

Amevitaja vyuo vilivyosajiliwa na kupewa vyeti  katika mkoa wa Njombe kuwa ni   pamoja na chuo cha matembwe vts ,the profesional college of njombe,  chuo cha lukungu vtc na kipengele vtc  igwachanya vtc

Kwa upande wao wamiliki na wakuu wa vyuo wameitaka Mamlaka hiyo  kuhakikisha inaonyesha meno yake kwa kuvifungia vyuo  visivyo na usajili ili kuwarahisishia wanafunzi kutokupata elimu isiyostahiki, na kukiri kuwa usajili huo walioupata utawapa chachu katika ufundishaji kwa mitihani itatungwa na mamlaka ya mafunzo na ufundi stadi VETA

Uongozi huo wa   mamlaka ya VETA kanda ya nyanda za juu umesema kuwa   usajili huo ni wa kwanza kwa mkoa wa Njombe  tangu kufutwa kwa usajili  wa vyuo vyote nchini kutokana na kuwepo kwa vyuo ambavyo havina sifa hivyo kuanza kusajili upya.

CHANZO:MFUGALE BLOG


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo