Baadhi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kutokana na kusababisha madhara ya kiafya.
Afisa
kutoka asasi ya Envirocare Bi. Ephrasia Shayo amesema hayo leo wakati
wa kampeni ya kuzuia matumizi ya vipodozi hatari inayoendeshwa na asasi
hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA.
Bi. Ephrasia ametaja baadhi ya madhara yanayotokana na matumizi ya
vipodozi hivyo kuwa ni saratanio ya ngozi, kuzaa watoto wenye ulemavu wa
akili, kuharibika kwa mimba, maelezo ambayo yameungwa mkono na
muelimishaji umma wa TFDA Bw. James Ndege.
Kwa mujibu wa Ndege, idadi kubwa ya vipodozi hivyo imeingia nchini
kwa njia za panya kutokana na hatua zinazochukuliwa na TFDA kudhibiti
uingiaji wa vipodozi hivyo katika mipaka.
Amesema watu wengi wanakimbilia kunua vipodozi hivyo kutokana na
kuuzwa kwa bei nafuu ambayo kila mwananchi anaweza kuimudu pasipo kujali
madhara anayoweza kuyapata.
Muelimishaji huyo kutoka TFDA amewataka wananchi kuchukua tahadhari
zote kuepuka matumizi ya vipodozi hatari, kama vile vyenye madini ya
zebaki, hydroquinone na nyinginezo ambazo zikiingia mwililini zinaleta
madhara makubwa kwenye viungo vya ndani ya mwili.
