NA KENNETH NGELESI,MBEYA
MAMLAKA ya Mapato nchini ,TRA, kitengo cha ushuru wa forodha
imeanza kutoa mafunzo kwa Mawakala wa Forodha na Watumishi wa Idara ya Forodha
mikoani juu ya matumizi ya mfumo mpya wa
utoaji wa mizigo kwa kasi katika Bandari na Mipaka ya nchi.
Mfumo huo unaujulikana kama (TANCIS) unakuja badala ya ule
wa zamani (ASYCUDA) na ukiwa mpango ambao umelenga kupunguza msongamano wa
magari ya mizigo mipakani, kuharakisha malipo ya ushuru na hivyo kuongeza kasi
ya kukua kwa uchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tunduma
Meneja
Msaidizi wa TRA Mkoa wa Mbeya kitengo cha ushuru na Forodha Joseph Ruge alisema
wanatoa mafunzo kwa watumishi 40 wa mamlaka hiyo na Mawakala 60 kutoka mpaka wa
Tunduma na kwamba umelenga kuwafikia Mawakala 1000 kutoka Mikoa ya Tanzania.
Ruge alisema kuwa mfumo huo ni kimtandao zaidi kwani mteja
ama wakala anaweza kufanya hatua zote na utoaji wa mzigo kutoka Bandari ya
Dar-es-salaamu akiwa nyumbani kwa kutumia simu ya Mkono imradi kuwe na mtandao.
Alisema kuwa mfumo huo ulianza kufanyiwa utafiti April mosi
mwaka huu kwa kushirikiana na watanzania na nchi ya Korea, ambapo Julai Mosi umeanza kufanyakazi
katika bandari ya Dar-es-salaam.
Akizungumza uamuzi wa kutoa elimu kwa mawakala katika Mpaka wa Tunduma na si mikoa
mingine Ruge alisema kuwa kutokana na umuhimu wa mpaka huo ambapo asilimi 70 ya
mizigo inayo pakuliwa katika bandari ya Dar-es-salaam inapitia mpaka huo kwenda
nchi karibu zote za kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kwa upande wake Sigsimund Kafuru Ofisa elimu na huduma
kutoka Makao Makuu ya TRA Muwezeshaji katika Mafunzo hayo Hilda mponzi walisema kuwa mfumo huo unafaidi
kubwa kwani ni wa uwazi na utaondoa udanganyifu katika masuala yote ya upakuaji
wa mizigo.
Alisema kuwa kumekuwa
nan tabia ya udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na vishoka ama wafanyakazi
wasio waaminifu juu kiwango cha malipo, na hatua ulipo fikia mzigo lakini kwa
kufanya hivyo mteja anaweza kujua malipo pamoja na hatua ulipo fikia.
‘Yahani mfumno huu utaondoa kabisa watu wanao jiita vishoka
kwani wamekuwa wakiwa tanganaya wateja juu,malipo pamoja na hatua ulipo fika
mzigo lakini kwa njia hii mteja anaweza kungalia kupitia mtandao na akafahamu
mzigo upofikia katika hatua ipi na malipo ni kiasi gani?’alihhoja Mponzi
Katika hatua ngingine Mponzi aliongeza kuwa faidi nyingine
ya kutumia njia hiyo ni kushirikisha tasissi zote ambazo zimekuwa zikihusika
katikia usarishaji na upakuji wa mizigoi ikiwe shirika na viwango (TBS),Mamlaka
ya Chakula na Dawa nchini (TRFA) ambapo taarifa zote zitafanyika kwa wakati
mmoja.
Baada ya Dar es salaam ambapo mfumo huu umeanza kutumika
Julai mwaka huu, TRA inautambulisha mfumo huu kwa Mawakala wa forodha wa Mpaka
wa Tunduma mkoani Mbeya na hii inatokana na mpaka huu kuwa na msongamano mkubwa
wa Magari ya mizigo ikilinganishwa na mipaka mingine nchini.
Meneja Msaidizi wa wa Forodha, TRA, Mkoa wa Mbeya Joseph
Ruge na mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo,Hilda Mponzi wanazungumzia mfumo huo
unavyofanya kazi kwa kuzihusisha pia Idara nyingine za serikali
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa
mafunzo hayo David Okechi ambaye ni mwenyekiti Mwenyekiti wa Makampuni ya Wakala Tanzania
alisema kuwa mfumo huyo utakuwa mkombozi kwao kwani utapunguza mizunguko ya
mara kwa mara na kwamba hatu zote za kupitisha mzigo zinaweza kufanyika akiwa
ofisini.
‘Katika hali ya kawaida ni wazi kuwa mfumo huu utatupunguzia
mizunguko isiyo ya lazima kwani kwa sasa
tunazunguka ofisi zote ili kupitisha mizogpo yetu lakini kwa mfumo huu mpya
taarifa zote tutazipata na kujaza kutia mtandao’alisema