KESI YA KUGOMBEA MAITI YAZIDI KUPAMBA MOTO MAHAKAMANI

MKE wa pili wa marehemu ,Stephen Assei (52) ,Fortunata Lyimo ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, kumpatia siku 14 kwa ajili ya kutafuta wakili atakayemsaidia katika kesi ya kugombea maiti.
 
Kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama hiyo na Lucy Laurant, anayetajwa kuwa ni mke wa marehemu wa ndoa.

Lyimo, aliwasilisha ombi hilo jana mbele ya hakimu wa Munga Sabuni, wakati wa kusikiliza shauri la usuluhishi wa mgogoro huo namba 39 la mwaka 2014.

Alidai kuwa hali yake kiafya si njema na anaiomba mahakama impatie siku 14 za matibabu pamoja na kumtafuta wakili.

Hata hivyo Upande wa mashitaka ukiongozwa na wakili wa serikali, Harold Njau, ulipinga ombi hilo kwa ukiwasilisha hoja mbili.

Hoja hizo ni aina ya kesi na kwamba muda ulioombwa na mshitakiwa kutafuta wakili ni mwingi kwasababu mawakili wako wengi.

Wakili Njau alidai kupanga siku 14 kutafuta wakili na kufuatilia matibabu katika kesi ambayo kimsingi inahusu maiti iliyofukuliwa ni kinyume cha sheria haki za binadamu Septemba 8, mwaka huu Mahakama hiyo iliamuru kufukuliwa kwa maiti ya Assei na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Kilema hadi hukumu ya nani kati ya wake zake wawili wanaolumbana ana haki kisheria ya kuzika.

Akisoma uamuzi mdogo wa mahakama, Hakimu Sabuni alisema imepokea pingamizi la mashitaka na kuamua Mshitakiwa awasilishe wakili wake ndani ya siku 7 .


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo