Gazeti la Mtanzania August 28 2014 ndio limeripoti hii stori kuhusu Bunge la Katiba linaloendelea Dodoma, kikubwa ni gharama mbalimbali zinazotumiwa na Wajumbe.
Wameandika
bunge la katiba lateketeza mamilioni ya fedha ambapo kikombe cha chai
na biskuti au karanga kinalipiwa shilingi elfu 10 kila siku kwa kila
Mjumbe mmoja licha ya kwamba kila Mjumbe anapokea posho ya siku ambayo
ni laki mbili na elfu 30.
Kwenye
sentensi ya pili wameandika, chakula cha mchana kila Mjumbe analipiwa
elfu 16 kwa siku ambapo kwa siku hiyohiyo iendayo kwa Mungu, ni shilingi
milioni 8 hulipwa kama gharama za ukumbi wa kufanyia mikutano.