Baba yake Beyonce Knowles, Mzee Mattew Knowles amefichua siri ya kuwepo ripoti kuwa mwanae anataka kuachana na Jay Z huku akigusia pia kuhusu kilichosababisha ugonvi kati ya Solange na Jay ndani ya lift.
Katika mahojiano aliyofanya na Roula &Ryan Show wiki hii, Mzee
Mattew alieleza kuwa anachofahamu ni kwamba tetesi hizo za talaka
ilikuwa mbinu ya kuuzia tiketi zaidi za tour yao.
Ameeita mbinu hiyo kuwa ‘Jedi Mind trick’ ambayo maana yake
ni nguvu ya kucheza na akili ya watu kwa kutengeneza utata fulani ili
kuwafanya wafikirie unachotaka kwa maslahi yako (kucheza na fikra zao).
“I know, because we’ve done this. From experience, there’s a tour
going on,So you sometimes have to ignite that tour. It’s called a Jedi
mind trick. The Jedi mind trick fools you a lot.” Amesema.
Alipoulizwa kuhusu ugomvi kati ya Jay Z na Solange, mzee huyo
aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa ile yote inaweza kuwa trick
ambayo imewasaidia pia katika tour hiyo hiyo na imesaidia kuuza albam ya
solange kwa asilimia kubwa.
“All I know is the Jedi mind trick. Everyone’s talking about it. Ticket sales went up. Solange’s album sales went up 200%!”
Katika hatua nyingine, jarida la OK limeripoti kuwa Beyonce ni mjamzito tena hivyo wawili hao wanatarajia kuwa na mtoto wa pili.
Kwa mujibu wa chanzo chao, tangu mwezi mmoja uliopita Beyonce amekuwa
akichagua vyakula kama alivyokuwa anafanya wakati anaujauzito wa Blue
Ivy na kwamba Jay Z amekuwa akihakikisha kwamba hapati stress yoyote.