Mtu mmoja ambaye inadaiwa kinara wa kuua na kujeruhi wanawake maarufu, wafanyabiashara na wenye vyeo katika ofisi mbalimbali jijini Arusha, Adamu Mussa (30) mkazi wa Majengo Juu jijini Arusha ametiwa mbaroni.
Mtuhumiwa
huyo ametiwa mbaroni juzi usiku na polisi na alipopekuliwa nyumbani
kwake alikutwa na bastola mbili na risasi saba na amekiri kuhusika
katika mauaji na kujeruhi wanawake jijini Arusha.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas, alizitaja bastola
mbili zilizokutwa nyumbani kwa mtuhumiwa moja ni aina ya Browning
iliyotengenezwa Jamhuri ya Czech yenye namba A 895936 na ilikutwa na
risasi saba.
Alisema
bastola ya pili aliyokutwa nyumbani kwake ni aina ya Lorsin yenye namba
za usajili 379126 iliyotengezwa nchini Marekani ikiwa na risasi tatu.
Sabas
alisema uchunguzi wa Polisi ulibaini kuwa bastola aina ya Browning
ilikuwa mali ya Seleman Bakari Msuya (33) mkazi wa Sombetini jijini
Arusha ambaye silaha yake hiyo iliibwa baada ya gari lake kuvunjwa kioo
siku za nyuma.
Wakati
huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo amewasihi wanawake kuwa
na moyo wa uvumilivu na kuacha vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi
zake ili kuwabaini wale wote wanaohusika na mtandao wa mauaji ya
wanawake pamoja na mtoto.
Mulongo
aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na
wanahabari wa vyombo mbalimbali ofisini kwake juu ya ujumbe uliosambazwa
kwenye simu mbalimbali kupitia mtandao wa Whatsapp kuhusu kujitokeza
kwa wanawake/wasichana leo kwa Mkuu huyo wa Mkoa ili kujua hatma yao.
Akizungumzia
suala hilo Mulongo alitoa rai kwa akinamama wote pamoja na wasichana
kuwa watulivu na kusaidia vyombo vya ulinzi na usalama kuwafichua wale
wote wanaofanya mambo hayo.
Awali
juzi watu saba walikamatwa jijini Arusha kwa tuhuma za kuhusika
kwenye mauaji ya unyang’anyi wa kutumia silaha kwa wanawake pamoja na
kusababisha kifo cha mtoto, Christen Nickos mwenye umri wa miaka
mitatu na nusu mkazi wa Olasiti jijini hapa.
Kamanda
wa Polisi Liberatus Sabas alisema watu wawili kati ya saba ambao ni
Japhet Lomnyaki (25) mkazi wa Sakina na Nehemia Kweka (34) mkazi wa
Ngaramtoni walifikishwa mahakamani juzi.
Huku
Adam Mussa (30) mkazi wa Majengo, Tito Loomoni (25) mkazi wa Shamsi,
Joseph Loomoni (29) mkazi wa Shamsi, Abdallah Maglan (202) mkazi wa
Oldadai na Emmanuel Maglan (23) mkazi wa Oldadai wakiwa wanaendelea
kuhojiwa na polisi.