Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Njombe, Fulgence Ngonyani na dereva wake, Nuaka Seme
wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Njombe ya Kibena baada ya kupata
ajali ya gari iliyomuua mlinzi wa kamanda huyo, usiku wa kuamkia jana,
eneo la kiwanda cha miwati (TANWAT).
Ngonyani
akizungumza hospitalini hapo, alisema ilitokea kati ya saa tatu na saa
nne usiku katika barabara ya Makambako -Njombe.
Alimtaja mlinzi wake
aliyekufa ajalini kuwa ni Konstebo George Stephano Matiko (24).
Naye
dereva Nuaka, alisema akiwa anaendesha gari la Polisi lenye namba za
usajili PT 2058 alivaana na lori ambalo dereva wake aliendesha akiwa
katikati ya barabara na baada ya kumwashia taa zote, alijaribu kuhamia
upande wake lakini hakufanikiwa kunusuru ajali baada ya kukwanguana.
“Mara
baada ya kukwanguliwa tulilikwepa lori tukaigonga nguzo ya umeme na
hapo hapo mwenzetu akafa na tunashukuru sana wafanyakazi wa kampuni ya
Tanwat ambao waliwahi kuja kutusaidia... na lile lori hatukuweza
kuchukua namba zake na liliendelea na safari.”