FAMILIA
moja ya Uturuki inawapasua kichwa wanasayansi, kutokana na wanandugu
watano kutokuwa na uwezo wa kutembea kama binadamu, na badala yake
wanatembea mithili ya wanyama, wakitumia miguu na mikono.
Hata
hivyo, katika uchunguzi wao wa awali, wanasayansi hao wameeleza kuwa,
hali iliyowakumba wanandugu hao haina uhusiano na mabadiliko ya
binadamu, kwamba wanaanza kurudi katika zama za mwanzo ambako inaelezwa
walitembea kwa miguu minne, wengine wakisema walianza kuwa nyani.
Ndugu
hao watano ambao ni kaka na madada, wakiwa na umri wa miaka 16 hadi 34
kutoka kijiji cha Jimbo la Hatay, kusini mwa Uturuki, walianza
kufuatiliwa na wanasayansi mwaka 2005 baada ya kugundulika na watu
kutoka nje ya kijiji chao.
Wanatembea kwa mtindo wa kutambaa kama dubu kwa mikono na wanaweza kusimama tu kwa muda mfupi, kwa magoti yao.
Utafiti
wa hivi karibuni ulifanywa na wanasayansi, Shapiro, Whitney Cole, Scott
Robinson na Karen Adolph, wote wa Chuo Kikuu cha New York, Jessica
Young wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Northeast Ohio na David Raichlen, wa
Chuo Kikuu cha Arizona.
“Lakini
hawa hawana uhusiano na mgeuko wa binadamu kwamba baada ya kupitia
hatua kadhaa za mabadiliko, sasa wanarudi katika hatua za awali, hilo
halipo,” mmoja wa wanasayansi hao amenukuliwa akisema.
Nadharia
za awali zilidai familia ya Ulas ilikuwa ikitembea kama nyani, na
kupendekeza kuwa huenda ni hatua ya kurudi nyuma kwa mabadiliko ya
binadamu.
Lakini
sasa, wanasayansi wa Kimarekani wamethibitisha kwa kusema wanandugu hao
wanakabiliwa na kasoro isiyoonekana na hutokea mara chache.
Katika
ripoti iliyochapishwa na PLOS One, watafiti walisema familia hiyo
wanatembea kwa namna tofauti kama nyani, ambao wakitembea huweka mikono
upande mmoja na miguu upande mwingine wakijirudiarudia.
Walidai kutembea kwa wanandugu hao ni matokeo ya hali ya kurithi ambayo husababisha uwiano wa akili kutatizika.
“Nilikuwa
na hamu ya kuweka rekodi sawa, kwa kuwa haya madai ya asili na sababu
ya kutembea kama mnyama wa miguu minne imechapishwa mara kwa mara, bila
kuwepo uchambuzi wa kwa nini wanatembea hivyo, na watafiti ambao si
wataalamu wa namna mamalia wa hali ya juu wanavyotembea,” Mtafiti Kiongozi Liza Shapiro wa Chuo Kikuu cha Texas alilieleza gazeti la The Washington Post.
“Tumeonesha
wanyama wa miguu minne wanavyofanana na mtu mzima mwenye afya njema
ambaye ameambiwa atembee kwa miguu minne wakati wa kufanya majaribio."
Mwaka
2005, watafiti wa Uingereza walikubali katika utafiti tofauti kuwa
utembeaji wa ndugu hao unatofautiana na baadhi ya mamalia wengine,
ikizingatiwa wenyewe hubeba uzito wao wote kwenye viganja vya mkono na
kifundo cha mkono na sio kiungio.
Hata
hivyo, Mtaalamu wa Bayolojia wa Uturuki, Uner Tan awali alidai
wanandugu hao, ambao pia wanaonekana kuwa wameathirika kwenye ubongo
wanakabiliwa na hali inayoitwa Uner Tan Syndrome.
Alisema
watu wanaokabiliwa na hali hiyo hutembea kwa miguu minne na mara
nyingine huzungumza kama wanyama na huwa na mtindio wa ubongo.
“Ghafla
nimegundua wanatembea kwa mtindo kama nyani kama walivyokuwa wahenga
wetu… nilikuwa wa kwanza kupendekeza kuwa kuna uwezekano wa hali ya
binadamu kugeuka na kurudi enzi za zamani za ubinadamu,” alisema.
Wandugu
hao ambao wazazi wao wanatembea kawaida, mara ya kwanza walirushwa
mwaka 2006 kwenye dokumentari ya BBC2, dokumentari hiyo ikiitwa The
Family That Walks On All Fours.
Wakati
mabinti wawili na mtoto mmoja wa kiume wamekuwa wakitembelea mikono
miwili na miguu miwili, mtoto mwingine wa kiume na kike mara nyingine
huweza kutembea wakiwa wamenyooka sawa, ingawa si kwa muda mrefu.
Profesa Nicholas Humphrey, ambaye aliitembelea familia hiyo mara mbili wakati wa dokumentari hiyo, alisema, “inashangaza
kama mfano wa kitu cha ajabu cha maendeleo ya binadamu. Lakini
kinachovutia ni jinsia wanavyoweza kuishi katika ulimwengu wa kisasa.”
Alisema
alifikiri familia hiyo imerudi katika silika ya mfumo wa tabia
iliyojikita ndani sana kwenye ubongo, lakini aliachwa wakati wa mageuko.
“Sidhani
kama walitakiwa kuwa wanyama wanaotembelea miguu minne kutokana na jeni
zao, lakini mfumo wa utengenezaji jeni zao zinawaruhusu kuwa hivyo,” alisema.
Wanandugu
hao watano ambao wana kaka na dada zao wengine 14 ambao hawajaathirika
na hali hiyo, hutumia muda mwingi kukaa nje ya nyumba yao ya familia
iliyoko kijijini. Hata hivyo, mmoja wao hutembea kijijini, kuchanganyika
na kuzungumza na watu.