Kweli dunia ina mambo! Kuna watu wanajaribu kutumia kila fursa inayopatikana kujinufaisha kwa kupata fedha hata ziwe ‘chafu’, kwao kitu cha maana ni kupata utajiri kwanza.
Kundi la watu wanaofanya biashara ya kusafirisha
watu, wamekuwa wakitumia fursa ya ukosefu wa ajira kama chambo cha
kuwanasa vijana na kuwaingiza kwenye biashara haramu kama ukahaba.
Hivi karibu kundi hilo linalosafirisha watu
lilipita katika vyuo vikuu kadhaa nchini Uganda na kuwaahidi wanafunzi
kuwa lingewatafutia kazi Ulaya na Marekani, kwani lina uzoefu wa kutosha
na kazi hiyo. Mmoja wa vijana ‘waliobahatika’ kupata nafasi ya kwenda
Ulaya kufanya kazi ni Sunday Bekunda (25), mwanafunzi wa mwaka wa pili
katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala.
Kwa bahati mbaya ‘neema’ ya kwenda Ulaya iligeuka
balaa baada ya kutekwa na kulazimishwa kufanya ngono na wanawake
mbalimbali huku akirekodiwa kwenye kamera za video.
“Ilikuwa ni Januari 2013, nilipokutana na mwanaume
mmoja anayeitwa Charles kutoka katikati ya Jiji la Kampala, ambaye
aliniahidi kunipeleka Kenya kufanya kazi katika kiwanda.
“Sikujua kuwa Charles alikuwa msafirisha watu. Alikuwa anaonekana kama mzazi wa makamo aliyefanya kazi kwa miaka mingi.
“Nilifungua moyo wangu na kumweleza changamoto
nyingi ninazopitia na namna nilivyo hangaika kutafuta kazi ili nipate
fedha za kulipia masomo ya ziada. Kwa kifupi ni kama nilikuwa namwambia
Charles kuwa sikuwa natafuta kazi bali nilikuwa nataka kazi yoyote.”
Safari ya Kenya
“Siku iliyofuata nilikuwa tayari kwa safari na
nilimkuta Charles akiwa kwenye gari la binafsi aina ya Toyota Noah.
Alikuwa pamoja na wasichana sita na wavulana wawili. Alituambia kuwa
tutaingia Kenya kwa kupitia mpaka usio rasmi unaoitwa Chepskunya.
“Tukiwa njiani, Charles alikuwa anaongea sana na
kutusisitizia kuwa ‘tusimwangushe’ tukifika huko.
“Tulipofika Kenya walituchukua na kutuingiza kwenye nyumba moja nzuri ya makazi ya watu, hapo tulikutana na wenzetu 15, wavulana wawili kutoka Rwanda na Wakenya 13.”
“Tulipofika Kenya walituchukua na kutuingiza kwenye nyumba moja nzuri ya makazi ya watu, hapo tulikutana na wenzetu 15, wavulana wawili kutoka Rwanda na Wakenya 13.”
Kutekwa
“Charles alituacha hapo tukiwa chini ya mwanamke
mmoja na wanaume wanne wenye miili iliyojengeka vyema. Watu hao walianza
kutupiga makofi na kutulazimisha tuvue nguo. Ndipo nilipobaini kuwa
kilichoonekana kama ni safari sasa imegeuka utekaji.
“Baada ya kupigwa tuliambiwa tutoe mifukoni kila kitu
tulichokuwa nacho na kuweka juu ya meza. Nilishtushwa nilipoona vyeti
vya wanafunzi wa Uganda kutoka Vyuo Vikuu vya Kyambogo, KIU (Kampala
International University), Nkumba na UCU (Uganda Christian University).
Hata vyuo vya Kenya vilikuwapo.
“Mwanamke alitutishia kutuua kama tusingetii
walichosema. Kudhihirisha alichokuwa anamaanisha, alituonyesha mkanda wa
video wa mtu akiuawa na kupasuliwa tumbo.
“Halafu wakaweka video vyingine iliyotuonyesha biashara tutakayokuwa tunaifanya, ambayo ni kuigiza picha za ngono.”
Ratiba ya kufanya ngono
“Walituongoza hadi ghorofa ya juu na kutuweka
katika vyumba tofauti. Katika chumba nilichokuwepo aliingia mtu na
kuniambia nitoe nguo kisha akanipa chupi tatu zinazobana.
“Hicho chumba kilikuwa na mwanga mkali na kamera
za CCTV katika kila kona. Baadaye wakamleta Bridget, mmoja wa wasichana
niliotoka nao Uganda, kisha wakaniambia kuwa nipo huru kufanya naye
ngono. Walipoondoka na kufunga mlango, Bridget alianza kulia na kupiga
kelele.
“Matukio mabaya yalianza rasmi siku iliyofuata
wakati yule mwanamke alipoingia kwenye chumba changu akiwa ameshika
mikanda mitatu ya ngono. Baadaye waliletwa wanawake na wanaume niliokuja
nao nikaambiwa nifanye nao ngono wakati watu wengine wakirekodi kwa
kutumia kamera kubwa.
“Nilipoishiwa nguvu, yule mwanamke alitoka nje na
kurudi halafu alinichoma sindano yenye dawa ambayo ilinifanya nipate
nguvu tena na kuendelea. Nikapewa ratiba ya kulala na wanawake asubuhi,
wavulana jioni (mashoga) na wanawake watu wenye umri mkubwa usiku.
“Wanawake hao walikuwa wanawalipa wale jamaa ili
tufanye nao ngono. Kuna wakati nilikuwa nalazimishwa kulala na wanawake
saba kwa siku huku nikipata maumivu makali.”
Mauaji
“Baada ya wiki tatu wote tuliitwa sebuleni na
kupewa taarifa kuwa mmoja wetu, aliyeitwa Sam Muteesi kutoka Uganda,
alikuwa amekataa kuwatii kwa hiyo alitakiwa auawe mbele yetu. Walimfunga
kwenye kiti, japokuwa alikuwa akiomba sana msamaha walimfunika usoni
kwa kutumia begi hadi alipokufa.
“Kwa kipindi chote cha Januari na Februari 2013,
nilikuwa nikifanya ngono za kila aina kila siku huku nikitumia dawa za
kulevya na pombe.
“Mwanzoni mwa Machi, Charles alikuja kwenye chumba changu na
kuniambia kuwa ninatakiwa kwenda kuoa Uingereza. Halafu akafungua
kompyuta yake na kunionyesha picha ya mwanaume mzee mzungu.
“Akaniambia nipite mbele ya kompyuta hiyo nikiwa nimevaa chupi nilizopewa ili huyo mzungu anione (kupitia Skype) kama ninafaa.
“Huyo mzungu alinipenda, hivyo Charles akawa
amepata ‘dili’ ambayo ingenipeleka Uingereza, lakini kwa kuwa sikuwa
Mkenya nilitakiwa nirudi Uganda kuchukua hati ya kusafiria.
Atoroka
“Wakati tukivuka mpaka kuingia Uganda, nilifanikiwa kukimbia pale Mbale
tulipokuwa tumesimama kunywa chai. Nilitoa taarifa yangu na kufunguliwa
faili namba SD REF 65/19/03/2013. Kwa kuwa Charles alikuwa mtu mwenye
nguvu (kifedha) hakufanywa chochote.
“Kutokana na mateso niliyopitia nilikuwa kama
kichaa, nililazwa katika Hospitali ya Vichaa ya Butabika na nilipewa
matibabu kati ya Agosti na Desemba 2013.
“Pia nilipimwa vipimo vingine na kugundulika kuwa
nilikuwa na maambukizi yote makubwa ya magonjwa ya zinaa.
“Nimeamua kusimulia habari yangu kama sehemu ya kampeni ya kuwaonya vijana wa vyuo vikuu kuwa makini na watu wanaowaahidi kuwatafutia kazi nje ya nchi.”
Credit: Mwananchi/ Redio Netherlands Worldwide (RNW)
“Nimeamua kusimulia habari yangu kama sehemu ya kampeni ya kuwaonya vijana wa vyuo vikuu kuwa makini na watu wanaowaahidi kuwatafutia kazi nje ya nchi.”
Credit: Mwananchi/ Redio Netherlands Worldwide (RNW)