Staa wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa na vituko, Aunt Ezekiel (katikati) akiwa karibu na dansa wa Wasafi Classic, Moses Yobo.
******
Staa wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa na vituko,
Aunt Ezekiel amenaswa live akijivinjari na mume wa mtu.******
Aunt alinaswa akiwa na mnenguaji wa Wasafi Classic, Moses Yobo
anayepiga mzigo chini ya Nasib Abdul ‘Diamond’ katika shoo ya Fiesta
iliyofanyika jijini Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba, wikiendi
iliyopita.
Wiki chache zilizopita, habari ya Aunt kufanyiwa vurugu nyumbani kwa Wema na mke wa
Yobo aliyekuwa na timu yake ilitawala katika mitandao ya kibongo.
Baada ya habari hiyo , Aunt aliibuka na kusema kuwa, hana
uhusiano wa kimapenzi na Yobo lakini kwa sababu amezushiwa, akaahidi
kujiweka karibu na kumfanyia mitego ili atoke naye kweli ndipo afanyiwe
vurugu ya halali.
Kuonekana akiwa naye jijini Mwanza, tena kwa ukaribu kama wapenzi
huku wawili hao kila mmoja akiwa hana mpenzi wake anayetambulika,
kulitafsiri kuwa Aunt ameamua kukinukisha.
Habari ambazo hazijathibitishwa kutoka kwa watu wa karibu na Aunt, zinasema kuwa, usiku huo baada ya shoo, wawili hao walilala pamoja katika hoteli ambayo haijajulikana.
Habari ambazo hazijathibitishwa kutoka kwa watu wa karibu na Aunt, zinasema kuwa, usiku huo baada ya shoo, wawili hao walilala pamoja katika hoteli ambayo haijajulikana.
Mwandishi wetu baada ya kuona hali na ukaribu huo alimfuata Aunt ili
kujua kama kweli ameamua kutekeleza azma aliyoitangaza, lakini akaruka
kimanga.
“Nimeamua kukaa na Yobo karibu ili kuwazingua wasanii ambao baada ya
kuniona wakawa wananitania eti mimi mkewe kutokana na taarifa za
magazeti zilizoripotiwa hivi karibuni, ila ukweli mwenyewe unaona tupo
hapa na Wema (Sepetu) na watu wengine na kimsingi hakuna kitu kibaya
kinachoendelea kati yetu,” alisema Aunt.
Chanzo: Risasi Mchanganyiko/ Gpl
Chanzo: Risasi Mchanganyiko/ Gpl