Biashara ya ngono iliyokithiri katika mji wa Morogoro imegeuka kuwa kero kwa wakaazi wa eneo hilo na familia zao hali inayowaweka hatarini zaidi watoto wadogo wasio na hatia wanaokutana na kondom zilizotumika huku mkuu wa Mkoa huo, Mheshimiwa Joel Bendera akinawa mikono kuhusu suala hilo.
Wakati hayo yakiendelea Morogoro, serikali kuu imekuwa ikitafuta dawa kali ya kuweza kudhibiti biashara hiyo hapa nchini.
Edson Mkisi Jr wa Times Fm, hivi karibuni alitembelea mkoa huo na
kushuhudia kushamili kwa biashara ya ngono sehemu mbalimbali za mkoa
wa Morogoro hususani katika maeneo ya Kaumba na Itigi mkoani humo.
Taarifa zilizopatikana awali toka kwa baadhi ya wakazi wa maeneo ya
mji wa Morogoro zilidai kuwa biashara ya ngono imekuwa kero mkoani
humo kutokana na utupwaji hovyo wa kondom zilizotumika katika mitaa
hiyo.
Kondom hizo zilizotumika zinahatarisha afya ya watoto wanaozitumia kama mapulizo.
“Kiukweli hii biashara mbali ya kutuaibisha sisi akina mama lakini
pia inatukera sana kutokana na utupwaji hovyo wa kondom unaofanywa na hao
akina dada….na baada ya kondom hizo kutupwa watoto wetu wanaziokota na
kuanza kupuliza kama maputo kwakweli inatukera sio siri,” anasema mama
Sakina mfanyabiashara maarufu wa samaki Msamvu Morogoro.
Baadae mwendesha bodabodo eneo hilo alimuonysha mwandishi wetu Hotel
moja maaufu na kudai kwamba Hotel hiyo imekodiwa na MALAYA hao kwa
ajili ya kufanyabiashara hiyo na serikali ya mkoa wanatambua ‘ishu’
hiyo!
“Yaani hawa akina dada wakiwa ndani ya hiyo Hoteli hakuna mtu
anayeweza kuwakamata ila wakifanya biashara yao nje ndio wanakamatwa na
polisi kwa huku Morogoro maarufu kama Voda Fasta,” anasema dereva
bodaboda huyo.
Kutokana na malalamiko mengi toka kwa wakazi wa Morogoro kuhusiana na
uwepo wa MALAYA hao katika viunga mbalimbali vya mkoa hao, Edson Mkisi
Jr, mtangazaji wa kipindi cha Hatua Tatu cha times fm, aliamua
kuwasiliana na Mkuu wa mkoa huo, Bw. Joel Bendara kwa ajili ya kujua
serikali ya mkoa inafanya jitihada gani katika kupunguza ama kumaliza
kabisa kero ya MAKAHABA hao.
Mkuu
huyo wa mkoa alidai kwamba hawezi kuzungumzia suala hilo la MAKAHABA
wala utupwaji hovyo wa kondom kwa maelezo kwamba suala hilo lina
hadhi ndogo sana ukilinganisha na cheo chake!
“Jamani hilo suala ni dogo sana kulingumzia mtu kama mkuu wa
mkoa….naomba ufuate protoko mimi siwezi kuzungumzia kondom ukilinganisha
na hadhi yangu hilo suala linamuhusu Mkuu wa Wilaya (DC), Meya ama
Diwani sio mimi jamani,” alisema Bw. Bendera.
Alipoambiwa kwamba yeye ni kama rais wa mkoa na si vibaya kuweza
kutoa neno kuhusiana na kero hiyo Mkuu huyo wa mkoa alisema; “Sasa hata
kama ni rais wa mkoa ndio najua kila kitu? Kwa hiyo hata Kikwete anajua
kila kitu kuhusu Morogoro? Ebu jaribu kuwa mtafiti kwanza hilo suala ni
la level ya chini sana kuna watu sahihi wa kuweza kuzungumzia sio
mimi…,” alisema Bendera.
Baada ya Mkuu huyo wa Morogoro ‘kumtolea mbavuni’ mwandishi wetu,
mwenyekiti wa serikali za mitaa, mtaa wa Mwanzo Mgumu, Bw. Said Omari
Kamba, mbali ya kukiri kukithiri kwa biashara hiyo, pia alikwenda mbali
na kudai kwamba eneo la Itigi pia ni kichaka cha wauzaji na wanunuaji wa
dawa za kulevya.
Credit: Times Fm