KESI YA TRAFIKI FEKI ALIYEKAMATWA JIJINI DAR YAAHIRISHWA TENA


Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imeendelea kupiga kalenda kesi ya aliyejifanya askari wa Usalama Barabarani, Jemes Hassan (45) kutokana na mshitakiwa huyo kuumwa.
 
Akiahirisha kesi hiyo jana, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Hassan Juma alisema shauri hilo litaendelea kusikilizwa Septemba 10, mwaka huu kutokana na mshitakiwa huyo kutofika mahakamani.
 
Kesi hiyo ambayo imefikia hatua ya kusikilizwa, imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara kutokana na sababu mbalimbali.
 
Tayari mashahidi wawili kutoka  Kituo cha Polisi cha Stakishari  wameshatoa ushahidi jinsi walivyomkamata Hassan akijifanya askari wa Usalama Barabarani.
 
Mshitakiwa huyo alifikishwa Mahakamani Agosti 14, mwaka huu, kujibu mashitaka ya kujifanya askari wa Usalama Barabarani baada ya kukutwa Kinyerezi Mnara wa Voda akiwa na sare za Polisi. Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na yupo rumande.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo