CHADEMA KUWAJADILI WABUNGE WASALITI WALIOHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kitawachukulia hatua kali wabunge wake iliyowaita kuwa ni wasaliti kwa kupuuza maagizo ya chama na kwenda kuhudhuria vikao vya Bunge Maalumu la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma.

Mkuu wa kurugenzi ya sheria ya CHADEMA na msemaji wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Tundu Lissu amesema hayo leo jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya chama hicho kutoa taarifa ya kuwepo njama za kutaka kukidhoofisha chama hicho.
 
Kwa mujibu wa Lissu, mamlaka ya nidhamu kwa wanachama wenye hadhi ya ubunge ni kamati kuu, chombo ambacho amesema ndiyo kilichotoa maagizo ya kwamba wajumbe wote wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA kutoka CHADEMA wasihudhurie vikao vya bunge maalumu la Katiba.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo