BAADA YA EBOLA KUUA WATU KONGO DRC, MKUU WA MKOA WA KIGOMA AAGIZA HAYA HAPA

Taarifa zinaarifu kwamba kati ya Wagonjwa nane waliokutwa na Ebola huko Congo DRC, wawili kati yao wamefariki dunia. 

Taarifa hizi zimeendelea kuwashtua na kuwafanya majirani kuzingatia tahadhari ambapo mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa Machibya amesema:
"Pamoja na tishio la ugonjwa huu kwamba uko DRC Congo (DRC ya mbali sana kule kaskazini wanakopakana na Afrika ya kati na Sudan), tumeanza kuchukua tahadhari kwenye mipaka yetu manake binadamu wanatembea na maingiliano ni makubwa.
 
‘Kuanzia leo nimemuagiza katibu tawala wa mkoa magari yote yenye uwezo wa kubeba vipaza sauti usiku au jioni watu wamesharudi nyumbani yapite kutangazia Wananchi kwa muda wa siku tatu mfululizo licha ya kuweka vipeperushi" 
 
John Ndunguru ambae ni katibu tawala wa mkoa amesema" "Kwenye hospitali zetu wameshatenga chumba maalum kama atatokea mgonjwa yeyote manake inabidi Wagonjwa hawa wawekewe kinga au wigo kwa siku 48, vilevile wizara ya Afya imeahidi kutuletea vifaa vya kutosha hasa vya kinga na dawa mbalimbali, tayari maafisa Afya wako hata uwanja wa ndege kukagua kila anaeingia"


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo