Katibu Mtendaji,
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (ORTM), Dkt. Philip I. Mpango, (wa tano kutoka
kushoto) akikagua Mradi wa Makaa ya Mawe Ngaka. Wengine ni viongozi na maofisa
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Shirika la Maendeleo la Taifa – NDC
pamoja na wataalam wa kampuni ya TANCOAL inayojishughulisha na uchimbaji wa
makaa ya mawe.
Viongozi na
Maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakiwa katika picha ya pamoja
na wataalam wa Kampuni ya TANCOAL ndani ya mgodi wa makaa ya mawe. Kampuni ya
TANCOAL ndiyo inayohusika nauchimbaji wa makaa ya mawe katika Mradi wa Mkaa ya
Mawe Ngaka.
Katibu Mtendaji
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Dkt. Philip I. Mpango (wa tatu kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango. Kutoka kushoto wengine ni Naibu Katibu Mtendaji Sekta za Uzalishaji
Bw. Maduka Paul Kessy, Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulika na Huduma za Jamii
na Idadi ya Watu, Bi. Florence Mwanri, pamoja
na wachumi kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Bi. Salome Kingdom, Bw. Erasmus
Masumbuko na Bw. Andrea Aloyce.
Viongozi na
maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na wale wa NDC wakipata maelezo
kuhusu mradi wa makaa ya mawe Ngaka kutoka kwa Mtaalam wa Kudhibiti Ubora (Quality Control Superintendent) Bw.
Boscow R. Mabena.
Viongozi na
maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC pamoja na wataalam kutoka
TANCOAL wakiwa katika eneo ambalo uchakataji wa makaa ya mawe unafanyika. 
Timu kutoka Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kikundi
cha Wanawake cha Mbalawala, Bi. Joyce Haule juu ya matumizi ya makaa ya mawe
majumbani. Makaa hayo hutumika majumbani kwa kutumia majiko maalum baada ya
kubadilishwa kitaalam na kuwa rafiki kwa matumizi ya majumbani. Mbalawala
kinajihusisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni jitihada za
kumkwamua mwanamke kiuchumi.
Majiko maalum
yanayotumia mkaa uliotokana na makaa ya mawe
kwa ajili ya kupikia majumbani.
Mtaalam wa
Kudhibiti Ubora, Bw. Boscow R. Mabena akitoa
maelezo namna ambavyo Coal Briquett
Machine (Pichani) hutumika kubadili makaa ya mawe kutoka hali yake ya
mwanzo baada ya kuchimbwa na kutengenezwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi