Mwenye
kiti wa Halmashauri ya kudhibiti vileo nchini Kenya NACADA bwana John
Mututho ameitaka michezo ya Ragbi ya Masaku 7s kupigwa marufuku na
serikali, pia wanamtaka gavana wa machakos DK. Alfred mutua kwa kukubali
watoto wadogo kuuziwa pombe wakati wa michezo hiyo.
Msururu wa
mechi za raga za wachezaji saba kila upande, hufanyika msimu kama huu
kila mwaka na hujumulisha masaku 7s ambayo inaandaliwa katika uga wa
Kenyatta mjini Machakos.
Baada ya
picha kadhaa kupandishwa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha matukio
ya masaku 7s mchana na usiku kucha kumekua na lalama kali kuhusu
mashabik kukosa kuonyesha maadili .
Wakati
wengine walikua wakiji starehesha kwenye eneo la burudani, msongamano wa
magari kati ya mji wa machakos makutano ya bara bara kuu ya
Mombasa-Nairobi iliyo chukua masaa 12, baadhi yao wakilala ndani ya gari
walipoamka wakajipata kwenye foleni bado.
Matukio
yalio wachukiza wengi ni picha zinazo waonyesha mashabik wakiwa
wanafanya mambo yasio semeka hadharani na kwa sababu hiyo wakuu kwenye
serikali wameanza kutoa hisia zao kuhusu wikendi ya Masaku 7s wa hivi
punde zaidi akiwa mkuu wa NACADA.
Mututho analinganisha kilichofanyika kwenye michi hizo za wikendi kuwa yalioshinda Sodom na Gomorrah.
Mwenye kiti huyo wa Nacada waandalizi wa michezo hiyo walivunja sheria kwa kuruhusu watoto kuuziwa pombe.
Anasema watoto wadogo wenye umri wa miaka 11 waliuziwa pombe kilicho wafanya watake kuchoma kanisa liloko karibu na uwanja huo.