Maji yawatesa wananchi Masasi

Na Casiana Ndimbo
Kutokana na kuwepo kwa tatizo la uhaba wa upatikanaji wa  maji safi na salama katika Kata ya Masasi wilayani Ludewa Mkoani Njombe limesababisha wananchi hao kutumia muda mwingi kutafuta maji katika visima vya asili ambavyo sio  salama.
 Akiongea na  mtandao huu  Alanus Mbunda Mtendaji wa Kata ya Masasi  amesema kuwa wananchi wa kata hiyo hawana huduma ya maji ya bomba kwa muda mrefu  badala yake wanatumia maji ambayo yanapatikana katika visima vya asili ambavyo sio salama kwa afya ya binadamu.
“ Maji tunayotumia kweli sio safi  na salama kwa afya zetu,tunachota katika visima ambavyo wakati mwengine hadi wanyama wanatumia visima hivyo hivyo suala la usafi kwa maji haya ni tatizo, pia visima hivyo tunavyovitegemea vipo mbali hivyo tunatumia muda wetu mwingi kutembea kutafuta maji tu kwa siku nzima” alisema Hilda Haule mkazi wa kiyogo.
Hata hivyo wananchi hao wamesema kuwa visima hivyo wakati wa masika havitoi maji  hivyo inawalazimu kutembea umbali wa masaa zaidi  ya manne hadi matano kutafauta visima ambavyo vinatoa maji jambo ambalo linawapotezea muda mwingi kutafuta maji badala ya kufanya kazi zao.
“Suala la kupata maji hapa kijiji ni tatizo kubwa, tumelipeleka jambo hili ngazi za juu lakini mpaka sasa  hatujaletewa jibu lolote, wakati wa kiangazi jukumu la kutafuta maji linakuwa la familia nzima hakuna anayebaki  nyumbani hali hii inarudisha nyuma maendeleo yetu kwani kwa kipindi hicho shughuli nyingi zinakwama”alisema Marko mitumba mkazi wa kijiji cha Lihagule.
Aidha Mtendaji wa Kata hiyo ameeleza kuwa kati ya vijiji vitatu vya kata hiyo kijiji cha kiyogo  wanatumia maji ya mto Ruhuhu na kijiji cha kingole na Lihagule wanatumia maji ya visimani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo