Hayo yalisemwa na Diwani wa kata ya Ligunga Bw. Kazembe Said kazembe wakati akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya baraza la idd mjini hapa na kuongeza kuwa endepo wataruhusu ujenzi huo kufanyika watakuwa wamechangia kuua mji wao.
Aidha Bw. Kazembe aliwaomba Wabunge hao kubadili mawazo hayo na kushirikiana na wananchi katika mapambano hayo na kuhakikisha kuwa Barabara hiyo inapitia mjini ili kuwawezesha wananchi wao kunufaika na Vipato vitakavyotokana na Magari yatakayo kuwa yakisafiri kutoka Pande za Namtumbo Mkoani Ruvuma na Mkoani Mtwara kupitia mjini Tunduru.
Wakifafanua taarifa hiyo kwa nyakati tofauti pamoja na diwani kazembe viongozi wengine ni wa Chama cha demokrasia na maendeleo Wilaya ya Tunduru ni Mwenyekiti wake Bw.Said Mwidadi na Katibu wake Bw. Nyenje Abdalah Hundi ambao walisema kuwa lengo la kujengwa kwa Barabara za Lami katika maeneo mengi hapa nchini nan chi zilizoendelea ni kusogeza huduma na kupeleka maendeleo kwa wananchi wanaoishi katika meneo husika hivyo kitendo cha baadhi ya Viongozi wakiwemo Wabunge wa majimbo ya Tunduru kuridhia ujenzi wa uchepushaji wa barabara hiyo na kuruhusu ipite nje ya mji unalenga kuendelea kudumaza maendeleo ya Wananchi wao.
Kufuatia hali hiyo Viongozi wa chama hicho wakamaliza kwa kuwataka wananchi kufanya maandalizi ya kutosha ili waweze kuchagua Viongozi wenye uchungu wa maendeleo katika maeneo yao tofauti na sasa ambapo wamekuwa wakichagua wawakilishi wanaoletewa na wajanja wachache ambao baada ya kuchaguliwa huyakimbia majimbo yao na kuwatelekeza wananchi na kuhamia mijini kwa visingizio vya kuwa na kazi nyingi.
Walisema mtindo wa Viongozi hao kuruhusu Barabara hiyo kupita njekwanje hautakuwa na manufaa kwa wananchi wa Wilaya hiyo hali ambayo itawafanya wabaki kuwa watazamaji wa shughuli za kimaendeleo kama ilivyo katika mji ya madaba,Iringa na hata morogoro ambayo miji yake ya asili imekufa baada ya watu kuihama kwa ajili ya kufuata maendeleo barabarani.
Katika Mkutano huo pia Viongozi wa cha chama hicho walikemea tabia za baadhi ya Viongozi waliopewa malaka Wilayani Tunduru kuondokana na mtindo wa kufanya kazi kwa mazowea pamoja na kushamiri kwa vitendo vya ulasimu hali amabyo imekuwa ikikwamisha upatikanaji wa huduma katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma kwa jamii.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo maeneo hayo ni pamoja na hospitali ya za serikali ambazo walidai kuwa pamoja na serikali kutoa maelekezo ya kutolewa kwa matibabu bila malipo kwa Wazee na watoto chini ya miaka mitano lakini wamekuwa wakiishia kuandikiwa vyeti na kuelekezwa kwanda kununu dawa katika maduka binafsi, ubovu wa huduma kwa akinamama amao hunda kwa ajili ya kujifungua katika zahanati, vituo vya afya na Hospitalini huku kukiwa na malalamiko ya akinamama hao kudharirishwa pindi wanapojifungua ambao wengi wao hulipotiwa kujifungulia katika makorido.
Na Steven Augustino wa demashonews, Tunduru