YULE MTOTO ALIYEFUNGIWA KWENYE BOKSI AFARIKI DUNIA


Nasrah Rashid (kulia) enzi za uhai wake. Mwanaume  mwenye  shati  la  bluee  aliyekaa ni baba yake mzazi Rashid Mvungi.
******
MTOTO Nasrah Rashid (4) aliyekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua na kupata ulemavu kwa kufungiwa kwenye boksi miaka minne amefariki dunia.
 
Nasrah alifichwa kwenye boksi na mama yake mkubwa aitwaye Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro tangu akiwa na miezi tisa baada ya mama yake mzazi kufariki
 Baba wa mtoto Nasrah, Rashid Mvungi (47) akiingizwa mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro baada ya kupandishwa kizimbani kujibu mashitaka ya kula njama na kufanya ukatili dhidi ya mtoto Nasra.
 Watuhumiwa wengine kwenye sakata hilo mama mlezi, Mariam Said (38) wa kwanza kushoto na mume wake Mtonga Omar (30) wa kwanza kulia wakisindikizwa mahabusu chini ya ulinzi wa polisi baada ya kusomewa mashitaka.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo