POLISI WAKIRI KUPOKEA TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA MUME WA FLORA MBASHA

Jeshi la Polisi limethibisha kupokea tuhuma za ubakaji dhidi ya mume wa mwimbaji wa injili Flora Mbasha anayefahamika kwa jina la Emmanuel Mbasha.

  Kwa mujibu wa Tovuti ya Times Fm, kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Ilala, Marietha Minangi ameeleza kuwa jeshi hilo limepokea tuhuma hizo kutoka kwa mlalamikaji ambaye ni binti mwenye umri wa miaka 17 na kwamba binti huyo alifika katika kituo cha polisi akiwa na ndugu zake.

“Taarifa zimepokelewa na zinachunguzwa. Taarifa zilizokuja ni za kubaka sasa tunazichunguza tufike mwisho tujue ni nini.” Kamanda Minangi ameimbia tovuti ya Times Fm.
 
Ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa mlalamikaji polisi walienda nyumbani kwake ambapo hawakumkuta yeye na mkewe na kwamba hadi sasa hawajapatikana.

Tovuti ya Times Fm ilitaka kupata ufafanuzi kuhusu uhusiano uliopo kati ya mlalamikaji na mtuhumiwa kwani taarifa za awali zinadai kuwa ni shemeji wa mtuhumiwa.

“Hayo yote yanachunguzwa, mimi siwezi kusema ni shemeji yake kabla hatujafikia mwisho wa uchunguzi. Tutakapofikia mwisho wa uchunguzi ndipo tutakapoweza kusema wana mahusiano gani.” Kamanda Minangi ameeleza.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo