UPELELEZI WA KESI YA WATUHUMIWA WALIOMTESA MTOTO NASRA HUKO MOROGORO BADO HAUJAKAMILIKA

Kesi ya watuhumiwa watatu wa unyanyasaji na kusababisha kifo cha mtoto Nasra Rashidi (4) imeahirishwa hadi Julai 10 mwaka huu, kufuatia upelelezi wa shauri hilo kutokamalika.
Wakili wa Serikali, Sunday Hyera, kwa kushirikiana na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Zabron Msusi, jana waliiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro kupanga tarehe ya kutajwa tena shauri hilo kufuatia upelelezi wake kutokamilika.

Hakimu Mary Moyo, alikubalina na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 10 mwaka huu.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana majira ya saa 3 asubuhi wakitokea mahabusu wakiongozwa na  baba mzazi wa mtoto huyo Rashid Mvungi (47) mkazi wa Lukobe pamoja na wanandoa Mariam Said (38) na Mtonga Omari (30), wote wakazi wa mtaa wa Azimio, kata ya Kiwanja cha Ndege, mkoani hapa.

Watuhumiwa wote walirudishwa rumande kutokana na kukabiliwa na shitaka la mauaji ambalo halina dhamana na mahakahama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.

Katika keshi hiyo, awali watuhumiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kula njama na kutenda ukatili dhidi ya mtoto Nasra.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Mei 26 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro baada ya mtoto huyo kufariki na watuhumiwa hao kubadilishiwa mashtaka na kusomewa la kusababisha mauaji.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo