UKAGUZI WA MAGARI ULIOFANYWA NA POLISI WASABABISHA ABIRIA KUTEMBEA KWA MIGUU MKOANI NJOMBE

Kufuatia jeshi la polisi mkoani Njombe kufanya ukaguzi wa magari ya kubebea abiria (daladala), kumepelekea usafiri kuwa mgumu baada ya baadhi ya wenye magari hayo kuyaficha na kusitisha huduma kukwepa kukaguliwa. 

Ukaguzi huo wa kushtukiza uliofanywa jana mkoani hapo umepelekea abiria wengi kutembea kwa miguu na wngine kulazimika kutumia taksi na pikipiki kuwapeleka maeneo mbalimbali wanayohitaji kwenda. 

Mwandishi wa mtandao huu wa eddy blog ameshuhudia daladala chache zikiwa zinafanya kazi kwa kubeba abiria huku vituo vikiwa na abiria wakisubiri usafiri na wengine kuamua kutembea kwa miguu. 

Mmoja wa abiria aliyezungumza na blog hii Bi. Jane Mwenda mkazi wa Kibena madukani amesema hamekaa kituoni kwa zaidi ya saa moja akisubiri daladala ili aweze kwenda Njombe mjini lakini toka amefika kituoni hajaona daladala. 

"Mimi sijaona daladala na sijui ni nini kimesababisha hii leo, hii si kawaida na kwa sasa itabidi nikodi bodaboda ama taksi ili nifike maada tumeambiwa daladala zinakwepa ukaguzi unaofanywa na polisi" amesema. 

Abiria mwingine aliyejitambilisha kwa jina moja la Mwalongo amesema ukaguzi huo mbali na kusababisha magari mengi ambayo yana makosa kujificha na usafiri kuwa mgumu, lakini askari hao wanafanya jambo jema kuhakikisha magari yanayofanya biashara yanakuwa kwenye mstari ulionyooka. 

Amesema wamezoea kuona askari wakikagua magari baada ya matatizo kujitokeza lakini hili la kufanya ukaguzi bila kusubiri matatizo yatokee ni jambo jema. 

Uchunguzi wetu pia umeshuhudia abiria wengi wakipanda kwenye mabasi yanayofanya safari masafa marefu ikiwemo Njombe Iringa ambayo yamekidhi vigezo kutokana na ukaguzi wake kufanywa mara kwa mara na nauli kupanda kutoka shilingi 400 ambayo imezoeleka na kufikia 500. 

"Mfano kutoka hapa Kibena mpaka stendi kuu pale unatozwa sh. 500 badala ya 400 na kama unaenda sehemu kama Hagafilo kule inabidi uchukue teksi ama bajaji napo ni hela tena, wakati kabla ya ukaguzi huu kutoka hapa kibena hadi Hagafilo ni sh. 400" amesikika mwananchi mmoja akiongea eneo la Ruhuji, 

Hadi mwandishi wetu anaondoka mkoani Njombe jana mchana, zoezi hilo bado lilikuwa likiendelea.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo