Waziri mkuu mh Mizengo Pinda amesema atazungumza na waziri wa mambo ya ndani kumuagiza kuhusu kero ya askari wanaotumia pikipiki maarufu kama "tigo" kuwabugudhi madereva pikipiki ili wachukuliwe hatua
Waziri mkuu Pinda ameyasema hayo bungeni katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo wakati akijibu swali la Mbunge wa Korogwe vijijini Mh. Steven Ngonyani kuhusu kero ya polisi hao
Katika swali lake amesema polisi hao wamekuwa wakiwakamata madereva bodaboda na kuwatukana pamoja na kuwatoza faini kubwa wakati mwingine bila kuwapa risiti jambo linaloweza kusababisha ugomvi usio na maana
Mh. Pinda amesema kwa kuwa mbunge huyo analifahamu tatizo hilo, atalipeleka kwa waziri wa mambo ya ndani kulifanyia kazi mara moja, ili polisi wa aina hiyo waweze kuchukuliwa hatua za kisheria baada ya kubainika kuwa ni kweli wamefanya kosa hilo