MTOTO aliyefahamika kwa jina la Najma Benjamin (7) amefariki dunia
papo hapo baada ya kugongwa na gari maeneo ya Bayuni Sheratoni, Kata ya
Chanika, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Ally Omary Mnzava, amesema kuwa
huko Barabara ya Chanika, gari aina ya Toyota Noah yenye namba T 611
CUN ikiendeshwa na Kasimu Ally (22) mkazi wa Chanika Mwisho, imemgonga
mtembea kwa miguu ambaye ni mtoto huyo.
Mnzava amesema mtoto huyo amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa
na gari, ambapo dereva kwa sasa amekamatwa na maiti kuhifadhiwa katika
Hosptali ya Taifa Muhimbili huku upelelezi ukiendelea.