Polisi wa dawati la Jinsia ambaye alipanda gari lililobeba mwili wa Nasra akishuka na Picha ya marehmu Nasra jana.
NA DUSTAN SHEKIDELE, MOROGORO.
Mvutano mkali
umezuka kwenye shughuri ya kuaga mwili wa Marehemu Nasra Mvungi kati ya
Polisi,maafisi Ustawi na Masheikh kuhusu picha ya marehemu Nasra
kuwekwa kwenye Jeneza wakati wa kuaga mwili wake kwenye Uwanja wa
Jamhuri Jana.
Maafasi wa
kike wa Polisi wa Dawati la Jinsia na maafisi wa Ustawi wa Jamii mkoa
walikuza Picha ya Marehemu Nasra kwa lengo la kuiweka kwenye Jeneza
jambo lililopingwa vikali na viongozi wa dini ya Kiislam wakida jambo
hilo ni kinyume na sheria za dini yao.
Hata hivyo
baada ya mvuta huo uliodumu kwa dakika 15 ulifikia muafaka baada ya
Polisi na maafisi Ustawi kupokea busara za mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Morogoro Mjini Bw Fikiri Juma aliyeingilia kati mvutano huo walikubali
kutoiweka Picha hiyo ya marehmu kwenye Jeneza,
Mmoja wa
mapolisi hao aliamu kuichukua kwa uchungu picha hiyo na kuiweka kwenye
mkoba wake huku akiseme” Kama wamekataa basi tutaenda kuiweka kwenye
Ofisi zetu kama kumbukumbu ya mtoto wetu Nasra”alisema kwa Uchungu
Afande huyo.
Akizungumza
kwenye hafra hiyo Kaimu Sheikh mkuu wa Mkoa wa Morogoro Sheikh Ally Omar
alisema Ingawa tukio hilo la kumuaga Nasra limefanyika Kiserikali
haimaanishi kuvunja sheria za dini kwa kuweka picha ya marehemu kwenye
Jeneza
“ Mbali ha
kuzia Picha hiyo kuwekwa Kwenye Jeneza laki pia Kisheria sisi hatuna
mambo ya kuga tukivunja sheria za dini nini nitaulizwa na wakubwa
zangu,hivyo kwa sasa sote tusimane na tutaga mwili wa Nasra kwa kusoma
dua na baada ya hapo tutaelekea msikiti kuuswalia mwili wa marehemu na
baadae kwenda kuuzika.
Marehemu Nasra
ambaye alifichwa kwenye Boksi kwa zaidi ya miaka 3 na mama yake Mkubwa
Bi Mariam Said alifichuliwa na wasamalia wema May 25 mwaka huu na
kutibiwa katika hospital ya mkoa wa Morogoro kabla ya kuhamishi hospital
ya Tifa Muhimbili ambako Jumapili iliyopita alifariki dunia na kuzikwa
jana makabuli ya mkoa mkoani hapa.
Kwa habari zaidi tembelea http://shekidele.blogspot.co.uk