Mhandisi Mwandamizi masuala ya uendeshaji katika Bwawa la Mtera, Mhandisi Julius Chomora akimweleza Naibu Waziri Nishati Mhe. Charles Kitwanga namna mtambo wa uendeshaji unavyofanya kazi. Anayefuatia ni Mhandisi Nishati Mwandamizi Wizara ya Nishati na Madini Salum Inegeja.
Kaimu Meneja wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Mtera, Mhandisi
Steven akimwonesha Mhe. Charles Kitwanga moja ya “Transfoma ‘’ iliyopo katika
eneo la Bwawa la Mtera.
======== ==========
Na
Asteria Muhozya, Mtera.
Naibu
Waziri Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati Mhe. Charles
Kitwanga amefanya ziara ya kutembelea Bwawa la kuzalisha Umeme la Mtera
mwishoni mwa wiki kwa lengo la kuangalia mwenendo wa maji katika bwawa
hilo.
Wakati
akizungumza na watendaji wa Bwawa hilo, Kitwanga amewataka watendaji hao kuhakikisha
kuwa Bwawa la Mtera linaendelea kuwa na kiasi cha maji ya kutosha wakati wote
ili kuweza kuzalisha umeme wa kutosha.
“Lazima
muhakikishe bwawa hili linakuwa na maji ya kutosha wakati wote. Hakikisheni
kuwa vyanzo vya maji ya bwawa hili vinakuwa endelevu”. Amesisitiza Kitwanga.
Aidha,
ameongeza kuwa, uzalishaji umeme kwa njia ya maji ni muhimu kutokana na gharama
zake kuwa nafuu ikilinganishwa na gharama za kuzalisha umeme unatokana na gesi
au vyanzo vingine. Hivyo, amewataka wananchi wanaofanya shughuli zao jirani na
vyanzo vya maji kuhakikisha wanavilinda kwa ajili ya maendeleo na manufaa ya
taifa.
Katika
hatua nyingine amewataka watendaji hao kufikiria vyanzo vingine vya kuzalisha
umeme mbali na gesi badala ya kusubiri rasilimali ya gesi pekee kuweza
kuzalisha umeme. “Tukumbuke
gesi inaweza kuisha, lakini kuna vyanzo vingine vingi ambavyo vinaweza kwenda
sambamba na gesi, lazima tuwe wabunifu”. Ameongeza.
Aidha
ameeleza kuwa, wananchi wana matarajio makubwa na nishati ya umeme hivyo,
amewataka watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kufanya kazi kwa bidii kwa
ajili ya kuwatumikia watanzania huku wakitanguliza uzalendo.