MWILI WA MAMA YAKE ZITTO, BI. SHIDA SALUM WASAFIRISHWA KWENDA KIGOMA KWA MAZISHI


Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe akiwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wakati wa kuuaga mwili wa mama yake kipenzi Bi. Shida Salum aliyefariki leo kabla ya kusafirishwa kwenda Kigoma kwa mazishi. Waheshimiwa wabunge na baadhi ya viongozi wakibeba jeneza lililobeba mwili wa marehemu mama yake Zitto Kabwe, Bi. Shida Salum kuingiza kwenye ndege tayari kwa safari ya kwenda Kigoma kwenye mazishi. Ndege ikiandaliwa ili kuweza kuingiza mwili wa marehemu mama yake Zitto Kabwe. Prof. Ibrahim Lipumba akijadili jambo na mwenzie baada ya kupakia mwili wa marehemu kwenye ndege kuelekea kigoma kwenye maziko.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, (Wakwanza kushoto), baba yake mzazi Zuberi Kabwe (Wakwanza kulia) na waombolezaji wengine, wakiomba dua kwenye msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam huku picha ya chini, waombolezaji wakiingiza jeneza lenye mwilki za Saida Salum, mama mzazi wa Zitto, Jumapili Juni 1, 2014. Mama yake Zitto, alifariki mapema saa 5 asubuhi, akiwa na umri wa miaka 64, kwenye hospitali ya AMI, Msasani jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu ya kansa ya kizazi.

Kwa mujibu wa Zitto, Saida ambaye hadi umauti unamkuta, alikuwa mwenyekiti wa Chama cah Walemavu nchini, mjumbe wa bunge maalum la katiba na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, atazikwa Jumatatu Juni 2, huko Mwanga-Kisangani baada ya sala ya mchana (Adhuhuri). Ameacha mume, na watoto 10, wanaume 6 na wakike wanne. alisema Zitto.
Picha zote kwa hisani ya Khalfan Said






JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo