KITUO CHA TV CHAFUNGIWA BAADA YA KUONESHA PICHA ZA RAIS MUSEVEN AKIWA AMESINZIA BUNGENI




Serikali ya Uganda imekifungia kituo kikubwa cha Televisheni cha nchi hiyo NTV kuripoti habari zozote zinazomhusu Rais baada ya kurusha hewani picha zinazomuonyesha Rais Yoweri Museveni amesinzia bungeni.
 
Mkurugenzi wa kituo cha habari za serikali Dennis Katungi amenukuliwa akisema: “Rais ana tabia zake wengi mnajua, huwa anatafakari na wanajua lakini bado wameonyesha picha hizo na kusema alikuwa amesinzia.”
 
Msemaji wa serikali Ofwono Opondo amethibitisha kuwa NTV Uganda itachukuliwa hatua za kinidhamu ambapo wameifungia kuripoti habari zozote zinazomhusu rais wakati bado serikali ikiangalia uhusiano wake na chombo hicho.
 
Ameituhumu NTV kwa kukosa utaalamu wa uandishi na kuegemea upande mmoja lakini hata hivyo hatua hiyo si ya kudumu ni ya muda tu kuwafanya wafikirie upya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo