BOMU LALIPUKA NA KUUA WATU WENGI KATIKA DUKA KUBWA LA MANUNUZI ABUJA NIGERIA

Video: Bomu lalipuka na kuua watu wengi katika duka kubwa la manunuzi Abuja, NigeriaShambulizi baya la bomu limeua idadi kubwa ya watu katika duka kubwa la manunuzi ‘Mall’ jijini Abuja, Nigeria.

AFP imeripoti kuwa bomu hilo limeripuka katika duka la manunuzi la Emab Plaza lililo karibu na Banex Plaza, maduka ambayo huwa na wateja wengi kuliko maduka yote (mall) katika jiji hilo.
“Unaona moshi mkubwa unafuka angani. Ni sehemu ya watu wengi.” Msemaji wa kitengo cha dharura cha Abuja aliiambia AFP.

Ripota wa Vanguard aliyekuwa kwenye eneo la tukio alisikika akiripoti kuwa anaona vipande vya miili ya watu katika eneo hilo na kwamba bado kuna watu wafanyabiashara wengi na watu waliotembelea Mall hiyo wamenasa kwenye jumba hilo.

Zaidi ya ambulance 6 zilionekana zikitoka kwenye eneo la tukio likiwa limejaza majeruhi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo