Watu sita wamepoteza maisha na wengine kumi na mbili wakijeruhiwa
kufuatia ajali iliyotokea eneo la Makongo barabara ya Bagamoyo jijini
Dar–es–salaam,ikiyahusisha magari manne mawili kati ya hayo yakiwa ni ya
abiria maarufu kama Daladala,zifanyazo safari zake kati ya
Ubungo,Mwenge,Makumbusho na Tegeta.
Vilio na simanzai vilitawala kwenye maeneo yanayozunguka hosipitali
kuu ya jeshi la wanachi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo jijini
Dar–es–salaam,ambapo mashuhuda wa ajali hiyo wanadai kuwa,dereva
aliyekuwa akitokea tegeta kwenda mwenge alikuwa katika mwendo wa kasi ya
ajabu.
Mganga mkuu wa hosipitali ya jeshi Lugalo iliyopokea majeruhi na
maiti hao,Brigedia Jenerali Dkt Makere Josiah,amethibitisha kupokea
majeruhi kumi na wawili na maiti sita,huku wengine hali zao zikiwa ni
mbaya na kukimbizwa kwenye hosipitali ya taifa ya rufaa Muhimbili kwa
matibabu zaidi.
