WATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA BANGI MKOANI MBEYA

Na Saimeni Mgalula,Mbeya
Jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia watu wawili kwa kukutwa na bhangi katika matukio mawili tofauti. 

Katika tukio la kwanza jeshi hilo linamshikilia Victor George (38) akiwa mkazi wa Kijiji cha Lupa Wilaya ya Chunya baada ya kukutwa akiwa na kete 15 za bhangi zenye uzito wa gramu 75.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa jana majira ya saa 12:50 mchana huko katika kijiji hicho Tarafa ya Kipembawe pia mtuhumiwa ni mtumiaji wa bangi

"Taratibu za kisheria zinafanywa ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani" alisema kamanda wa polisi mkoani hapa kamishina msaidizi wa Jeshi hilo Ahmed Msangi.

Na katika tukio la pili anashikiliwa Maneno Msaru (25) Mkazi wa kijiji cha Mabadaga kilichopo Wilaya ya Mbarali Mkoani hapa,baada ya kukamatwa akiwa na kilo 15 Za bangi na baiskeli tatu aina ya bambucha mali inayodhaniwa ni ya wizi.

 Kamanda Msangi akithibitisha tukio hili alisema kuwa mtuhumiwa alikamatwa jana majira ya saa 9:00 mchana kijijini hapo kata ya Chimala Tarafa ya Rujewa Wilayani hapa pia naye alikuwa ni mtumiaji wa bangi

Kamanda wa Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha kujihusisha na madawa ya kulevya kwani ni kinyume cha sheria.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo