Kufuatia adha waliyokuwa wakiipata wananchi wa kijiji cha Tandala kata ya Tandala wilayani Makete mka wa Njombe wakati wa kuvuka eneo hili, imewalazimu wananchi hao kuchukua hatua na kutumia nguvu zao kujenga daraja hili
Hapo awali mto huu ulikuwa na daraja ambalo lilikuwa limechoka na kusababisha maji kupita juu ya daraja na mengine yakizagaa pembeni na kusababisha wapitaji kushindwa kupita hasa msimu huu wa mvua za masika
Picha zote hapo juu zinaonesha jinsi daraja hilo lilivyojengwa kwa nguvu za wananchi, na kwa sasa maji yanapita muda wote hakuna tena kero
Tazama picha hizi hapa chini uone hali ilivyokuwa mbaya kabla ya wananchi hao kuamua kuchukua hatua




