Kikosi cha kitulo fm kilichoanza mtanange huo.
Kikosi cha VETA Makete kilichoanza mtanange huo.
Mtanange ukiendelea.
Golikipa wa Kitulo Fm Aldo Sanga akifurahia kutoka droo.
=======
Mtanange uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki mbalimbali kati ya timu ya kituo cha redio cha Kitulo Fm na chuo cha VETA Makete umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Mtanange huo Uliopigwa katika dimba la Kabinda wilayani hapa ulikuwa ni wa vuta nikuvute huku kila timu ikihsmbulia kw zamu lango la mwenziye bila mafanikio.
Mchezaji wa Kitulo FM ajulikanaye kama Malafyale alizawadiwa kadi mbili za njano ambapo ilizaa nyekundu na kulazimika kutoka nje ya uwanja dakika chache kaba ya mpira huo kumalizika.
Hadi refarii Faustine Hunja anapuliza kipyenga cha mwisho, Kitulo Fm 0 na VETA Makete 0