TAARIFA ZA AWALI KUHUSU KIFO CHA ADAM KUAMBIANA

Marehemu Adam Kuambiana akiwa location enzi za uhai wake.

 Hizi ni taarifa zingine za ghafla ambazo Tanzania tumezipokea kwa mshtuko na masikitiko ni kifo cha miongoni mwa-madirector wa Tanzania ambao ni waigizaji pia,huyu ni Adam Kuambiana ambaye taarifa za kifo chake zimeanza kusambaa mchana wa Mei 17.

Mwenyekiti wa Bongo Movie Steve Nyerere amesema>>’Mwenzetu Adam Philipo Kuambiana amefariki akiwa Location ana shoot,mimi nimepigiwa simu saa 3 asubuhi kuwa hospitali pale Mwenge niende nikahakikishe kuwa ni kweli Adam amefariki na kweli kufika pale nikamkuta Adam Kuambiana amefariki’

‘Sasa hivi tumetoka Muhumbili kwenda kumsitiri mwenzetu,taarifa inasema wakati yupo location alikua analalamika tumbo linamuuma linamuuma kumfikisha hospitali ndipo umauti ukamfika’.

Kwa mujibu wa Steve Nyerere amesema kuwa marehemu Adam kuambiana alikua ana shoot filamu yake mpya ambayo ndani yake amewashirikisha wasanii kadhaa wa Bongo fleva akiwemo Q Chillah,


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo