Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama amekanusha vikali taarifa zilizozagaa mitaani kuwa kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki wa nyimbo za Injili Rose Muhando
Msama amesema hana mahusiano yoyote ya kimapenzi na Rose Muhando na wala hajawahi kutembea naye siku za nyuma mpaka leo hii
"Kiukweli nataka kusema mbele yenu hapa. sijawahi kuwa na mahusiano yoyote ya kimapenzi na Rose Mhando, wala msanii yoyote ambaye "ninampromote", hata kumbusu sijawahi, ila nina mahusiano naye ya kawaida tu kama promota wake" amesema Msama
Msama ameyasema hayo kwenye kipindi cha Mkasi kinachorushwa na kituo cha televisheni cha EATV wakati akijibu swali aliloulizwa kuhusu mahusiano yake na Rose Muhando
Amesema suala hilo limemuathiri kiasi kikubwa hasa kwa upande wa familia hivyo kumwambia mkewe ambaye ameathiriwa na taarifa hizo kufanya uchunguzi wa suala hilo na akibaini kuna ukweli yupo tayari kuwajibika kwa hilo
