Miongoni mwa stori za mjini zilizobamba wikiendi hii ni hii ya Mamba kuuawa Block 41 Kinondoni Dar es salaam kwenye eneo ambalo wanaishi watu kadhaa maarufu wa Tanzania akiwemo Kalapina wa kikosi cha Mizinga, hii ni nyuma ya bestbite, Mamba huyu akiwa ametokea kwenye bwawa nyuma ya 41 Records.
Bwawa limezungukwa na nyumba kwenye eneo la kwa Kisamo zamani Kajima
ambapo kwenye hili bwawa zamani kidogo kulikua na Mamba wawili ila baada
ya kugundulika mmoja alichukuliwa na watu wa Wanyama ila mwingine
hakuonekana.
Tukio
la juzi ilikua saa nane usiku ambapo mamba huyu alijitokeza barabarani
mtaani ndipo majirani wakamuita mtu mwenye bunduki kwenye huo mtaa
ili amuue kwa sababu mwanzoni kabla hawajajua walikua wanahofia kumuua
wakidhani ni kosa la kisheria.
Baada
ya kuuwawa kwa risasi nne, Defender ya Polisi ilikuja na kumchukua huyu Mamba

