SERIKALI YASEMA HAINA MPANGO WA KUTUNGA SHERIA YA KUWANYONGA HADI KUFA WAHUJUMU UCHUMI

Serikali imesema haina mpango wa kutunga sheria ya kuwanyonga hadi kufa wezi ama wahujumu uchumi wa nchi. 

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo hii na waziri wa sheria na Katiba Dkt. Asha Rose Migiro wakati akijibu swali la mbunge wa Kasulu mjini Mh. Moses Machali. 

Dkt Migiro amesema adhabu ya kifo imekuwa ikitekelezwa kwa waliobainika na baadhi ya makosa ikiwemo mauaji, lakini kwa sasa serikali haina mpango wa kutunga sheria ya kuwanyonga wahujumu uchumi.

Katika swali la Mh. Machali limeeleza kuwepo kwa matukio mbalimbali ya kuhujumu uchumi ikiwemo barabara kujengwa chini ya kiwango lakini waziri Dkt Migiro kufafanua kuwa yapo makosa yaliyoainishwa kisheria kuwa ni ya uhujumu uchumi hivyo mamlaka husika zikibaini makosa hayo kama ni ya uhujumu uchumi hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo