Msanii wa Bongo Fleva AY akiwa amewasili na crew yake nzima mkoani
Morogoro kumpa pole Mboni Masimba, AY alitoa mchango wa shilingi laki
sita kununua jeneza la marehemu Tyson hii ikiwa kama mchango wake kwa
kuthamini kile alichomfanyia wakati akiwa hai.
Sasa msafara unaelekea Dar Es Salaam na mwili utafikia Hospitali ya
Kairuki iliyopo Mikocheni na msiba utakuwa upo Bahari Beach nyumbani kwa
marehemu.
Picha: Dj Choka