skip to main |
skip to sidebar
PICHA NA HABARI KAMILI KUHUSU KUUAWA KINYAMA KWA AFISA USALAMA WA TAIFA JIJINI DAR
MAJONZI mazito yameikumba Ofisi ya Rais, ikulu
jijini Dar es Salaam kufuatia kutokea kwa vifo viwili vya watumishi wa
ofisi hiyo wiki iliyopita.
Picha ya marehemu Rashidi John Chilwangwa (45).
Wa kwanza ni Afisa Usalama wa Taifa Mwandamizi, Silvanus Adriano
Mzeru (56) aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Aprili 29,
mwaka huu maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,
Dar.
Picha ya Marehemu ambaye alikuwa Afisa Usalama wa Taifa Mwandamizi, Silvanus Adriano Mzeru (56).
Gazeti hili lilifuatilia habari hiyo na kunasa madai kwamba wauaji
hao walikuwa na pikipiki aina ya Boxer. Ilielezwa kuwa wadunguaji hao
walimfuatilia afisa huyo tangu maeneo ya Tazara jijini Dar.
Ilidaiwa kuwa, kufika eneo hilo la uwanja wa ndege, taa za kuongozea
magari zilionesha ishara ya magari yanayotokea mjini yanatakiwa
kusimama lakini baada ya dakika kama mbili taa hizo ziliruhusu magari
kuondoka.
MKe wa Silvanus Mzeru kushoto pichani.
Ndipo ghafla watu hao waliokuwa wamejibanza sehemu walimmiminia
risasi marehemu upande wa mbele wa kioo na kumfanya apoteze uelekeo
na gari lake aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T
844 CUG kwenda kuligonga kwa nyuma gari lingine lenye namba T 786
BLS.
Mama Salma Kikwete (mbele) na akina mama wengine wakiwa katika hali ya majonzi.
“Cha ajabu sasa, baada ya kufanya kitendo kile, wale watu kwanza
walipiga risasi hewani ili raia wasisogelee eneo la tukio. Halafu
ndani ya gari la marehemu walikuta pesa ambazo kiwango chake
hakijafahamika na ‘brifkesi’ inayodaiwa ilikuwa na nyaraka mbalimbali,”
kilisema chanzo.
Ukiachana na mauaji ya afisa usalama huyo,
mfanyakazi mwingine wa ikulu, Rashid John Chilwangwa (45) naye alikutwa
na mauti baada ya kuanguka ghafla.
Mwili wa Silvanus Mzeru wakati akisindikizwa kwa safari yake ya mwisho.
Chilwangwa alifariki dunia ghafla saa 4:20, Mei Mosi, 2014 ndani ya
Uwanja wa Uhuru wakati sherehe za siku ya wafanyakazi duniani
zikiendelea.
Waandishi wa habari walikuwepo katika eneo la tukio na kushuhudia
wafanyakazi wa ikulu na wananchi wengine wakitokwa machozi mara baada ya
kupokea taarifa za kifo hicho kutoka kwa wafanyakazi wa Msalaba
Mwekundu waliokuwa wakijaribu kuokoa uhai wake.
Baadaye ilidaiwa kuwa, marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari na siku ya tukio, presha yake ilipanda.
Mwili
wa Chilwangwa uliagwa Ijumaa iliyopita nyumbani kwake, Mabibo jijini
Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo mke wa rais,
mama Salma Kikwete ( pichani).
Marehemu Chilwangwa alizikwa
Ijumaa hiyohiyo, Kisarawe, Pwani huku marehemu Mzeru akizikwa Mei 3,
mwaka huu kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mungu azilaze pema peponi, roho za marehemu hao. Amina.
CHANZO: GAZETI L UWAZI VIA GPL
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi