Maalim Seif akishiriki katika mazishi ya Sheikh Ilunga Shekh Hassan Kapungu yaliofanyika katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni Dar es Salaam
Sheikh Ilunga Shekh Hassan Kapungu enzi za uhai wake
Wananchi wakishiriki katika mazishi ya Shekh Ilunga Hasaan Kapungu katika makaburi ya Magomeni Mwinyimkuu jijini Dar-es-Salaam.(Picha na Salmin Said OMKR)
******
Na Hassan Hamad.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
amewaongoza maelfu ya waislamu katika mazishi ya sheikh maarufu wa Mkoa
wa Mwanza na mwanaharakati wa dini ya Kiislamu marehemu sheikh Ilunga
Hassan Kapungu.
Sheikh Ilunga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam na kuzikwa katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.
Katika
uhai wake, sheikh Ilunga Kapungu alikuwa mwanaharakati ambaye mara
nyingi alikuwa akiendesha mihadhara ya wazi ya dini ya Kiislamu, ambapo
mwishoni mwa mwaka 2013 alikamatwa mkoani Tabora
na baadaye kuachiwa huru kwa tuhuma za uchochezi wa
dini kupitia kanda za CD na VCD zilizokuwa zikiuzwa kwa waumini ili
kueneza chuki na ukabila ikiwemo kuhimiza kuwachinja mapadri.
Kwa
mujibu wa taarifa za kimtandao, kabla ya kukamatwa kwake na kuachiwa
huru Disemba mwaka 2013, marehemu sheikh Ilunga alikwenda nchini India
kwa matibabu baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo pamoja na sukari.
Akizungumza
katika mazishi hayo , sheikh Basaleh wa Dar es Salaam, amesema marehemu
sheikh Ilunga alikuwa mwanaharakati imara na ni mfano mzuri wa kuigwa
katika harakati za dini ya Kiislamu.
Mazishi
yake yameweka historia baada ya maelfu ya waislamu kujitokeza
kushiriki, hali iliyopelekea mchanga wa kaburi lake kufukiwa kwa mikono
badala ya kutumia mapauro na majembe kama ilivyozoeleka.
Masheikh kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania wameshiriki mazishi hayo akiwemo sheikh Kishk





