MUHIMU: HIZI NDIO DALILI ZA HOMA YA DENGUE

Homa ya Dengue ni ugonjwa unaoenezwa kwa kuumwa na mbu aina ya Aedes mwenye virus vya ugonjwa huu. Mbu hupata virusi vya homa ya Dengue anapomuuma mtu mwenye ugonjwa huu.

Ugonjwa huu unaenezwa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine kwa kuumwa na mbu huyu.
 
DALILI:
 
Homa kali ya ghafla
Kuumwa kichwa hususani sehemu za machoni
Maumivu makali ya viungo na misuli ya mwili
Kichefuchefu au kutapika
Kutokwa na damu kwenye fizi, na sehemu za uwazi za mwili.
Uchovu
ukimsikia ndugu au jamaa yako anasema kuwa na dalili hizi muwahishe hospitali mapema. 
 
SAMBAZA UJUMBE HUU ILI WATU WAJUE


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo