MTOTO AFUNGIWA KWENYE BOKSI KWA MIAKA MINNE HUKO MOROGORO


Mkazi wa Mtaa wa Azimio, Kata ya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro,
Mariam Said ( kati kati) akizindikizwa kwenda Kituo Kikuu cha Polisi na
Askari Polisi wa kike ,juzi ( Mei 20)  baada ya kutoa maelezo kwa Ofisa
Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu ( hayupo pichani)
kutokana na madai ya kufanya vitendo vya ufanyasaji na ukatili  mtoto wa
mdogo wake  baada ya kufariki dunia, kwa  kulea mtoto, huyo wa kike mwenye
umri wa miaka ninne  ambapo yenye na mumewe , Mtonga Omary ,( hayupo
pichani)  walipoamua kumfungia  chumbani  na kwenye   boski  kwa muda miaka
yote hiyo.
Mkazi wa Mtaa wa Azimio, Kata ya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro, Mtonga Omary ( kati kati) akizindikizwa kwenda Kikuu cha Polisi na Askari Polisi wa kike baada ya kutoa maelezo kwa Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu ( hayupo pichani) kutokana na madai ya kufanya vitendo vya ufanyasaji na ukatili yeye na mkewe Mariam Said ( hayupo pichani) kwa kumfungia chumbani na kwenye bokis mtoto wao wa kike wa kumlea mwenye umri wa miaka minne.


Askari Polisi wa Kike ( kushoto) ambaye jina lake hakikuweza kufahamika mara moja akimwesha juisi ,mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne ( jina linahifadhiwa) aliyekuwa amefungiwa ndani ya chumba kwa kipindi cha muda wa miaka minne na kukaa ndani ya boksi kwenye nyumba iliyopo Mtaa wa Azimio, Kata ya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro, ( wapili kushoto) ni mama mlezi Mariam Said ( kati kati),ni baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi na ( kulia) ni baba mlezi wa mtoto , Mtonga Omary, hapawalikuwa wakitoa maelezo mbele ya Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu ( hayupo pichani).


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo