Maandamano ya wafanyakazi wilayani Makete mkoani Njombe yakitoka kwenye ofisi za halmashauri ya wilaya hiyo.
Mwendesha bodaboda Fadhili Ilomo na wenzake wakinogesha maandamano hayo.
Bango la idara ya ujenzi wilayani Makete kama linavyoonekana.
Madereva bodaboda wakikata mitaa Makete mjini.
Hata watoto hawakukosa maadhimisho hayo.
Askari wakiongoza wafanyakazi kuingia viwanja vya mabehewani yalipofanyika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani.
Waalimu wakipita mbele ya mgeni rasmi katika viwanja vya mabehewani.
Watumishi wa idara ya afya wakipita mbele ya mgeni rasmi.
Wafanyakazi wa idara ya kilimo, wakipita mbele ya mgeni rasmi.
Madereva bodaboda wakipita na bango lao mbele ya mgeni rasmi.