MASHUA ZISIZOTUMIA INJINI ZAPIGWA MARUFUKU KUVUSHA ABIRIA KWENDA NG'AMBO YA BAHARI LINDI NA MTWARA

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) mkoani Lindi, imewataka wamiliki wa Mashua zisizotumia Injini kuacha kuvusha abiria kwenda ng’ambo ya Bahari, kwa kuwa hali hiyo inahatarisha maisha ya abiria. 

Agizo hilo limetolewa  na Mkaguzi wa vyombo vya majini katika mikoa ya Lindi na Mtwara, Galas Chambo, kufuatia Manahodha wa Mashua hizo kubainika kuvusha abiria kutoka mji wa Lindi kwenda kwenye eneo la Kitunda katika Manispaa ya Lindi.
 
Aidha, amesema vitendo hivyo ni hatari katika maisha ya wananchi wa eneo hilo na maeneo mengine, kwani vinaweza kusababisha ajali, kutokana na vyombo vyao kutokuwa na Injini wala vifaa vya kujiokolea. Amesema mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani humo limeanza kuendesha msako wa kukamata vyombo hivyo, vinavyo kiuka sheria na taratibu za mamlaka hiyo.
 
Kwa upande wake mwakilishi wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Mkaguzi msaidizi wa Polisi, Baraka Masata, amesema kuwa Jeshi hilo limeitaka (Sumatra) kutoa elimu kwa wamiliki na Manahodha wa vyombo hivyo ili waweze kutambua madhara yanayoweza kusababishwa na vitendo vya kuvusha abiria bila kuwa na vifaa vya usalama.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo